Rais wa Marekani, Donald Trump anatarajiwa kukutana na Viongozi wa mataifa saba yenye nguvu za kiuchumi duniani maarufu kama G 7 kwaajili ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu ulinzi na usalama.

Mkutano huo unatarajiwa kuwa ni wa siku mbili ambapo viongozi hao watajadili masuala ya kiuchumi, ulinzi na usalama pia changamoto kubwa ambazo zimekuwa zikiukabili umoja huo hasa ugaidi na masuala ya kiuchumi.

Wakuu hao wa mataifa yenye nguvu duniani unafanyika Sicily nchini Italy na utakuwa wa kwanza kuhudhuriwa na Rais Trump katika siku yake ya mwisho ya ziara yake ya nchi za nje.

Vile vile, mkutano huo unafanyika pia wiki hii ambayo mashambulio ya kigaidi yamefanyika nchini Uingereza, huku viongozi hao wakitarajiwa kukubaliana juu ya haja ya kuongeza mapambano kukabili imani kali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *