Rais mteule wa Marekani, Donald Trump ametangaza kuwa ataacha kufanya biashara kabisa kutokana na majukumu yake ya urais wa Marekani.

Katika ujumbe aliotuma kwenye mtandao wake wa kijamii wa twitter, Trump amesema licha ya kuwa hashurutishwi kuchukua uamuzi huo, amedhani ni hatua muafaka ili kuzuia mgongano wa maslahi.

Trump amesema atatoa maelezo zaidi mwezi ujao akiwa na wanawe katika kikao na waandishi wa habari.

Wakati huo huo Trump amemteua afisa wa zamani za kampuni ya Gold maan sach, Steven Mnuchin kuwa waziri wake wa fedha.

Mnuchin mwenye umri wa miaka 53 aliongoza operesheni za kifedha za trump wakati wa kampeini.

Uteuzi huo hata hivyo unahitaji kuidhinishwa na bunge senate.

Bw Trump na maafisa wake wa mpito bado hawajaidhinisha uteuzi huo ambao ulitajwa na wingi kupitia uvumi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *