Rais mteule wa Marekani, Donald Trump amezionya vikali kampuni ambazo zinataka kuhama nchini Marekani baada ya kushinda kiti cha urais wa taifa hilo.

Trump amesema hayo katika jimbo la Indiana ambapo alijisifu kwa kunusuru kazi 1000 katika kampuni ya Carrier Corp ambayo ilikuwa inapanga kuhamia Mexico.

Bw Trump sasa yuko katika jimbo la Ohio kuanza ziara ya kutoa shukrani kwa wafuasi wake.

Kiongozi huyo ameunga mkono mazungumzo na kampuni ya Carrier Corp kama mfano wa vile atakavyoshirikiana na wafanyibiashara wengine wanaotaka kuhamia mataifa mengine.

Pia aliahidi mpango wake wa kampeni wa kupunguza kodi miongoni mwa biashara nchini Marekani.

 

                                                                                           

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *