Rais wa Marekani, Donald Trump ameweka masharti mapya ya maombi ya Visa kutoka kwa mataifa sita ya Kiislamu pamoja na wakimbizi wote.

Masharti hayo yanawataka kuwa na mtu wanaohusiana ama ushirikiano wa kibiashara na Marekani.

Hatua hiyo inayoyahusisha mataifa yalio na Waislamu kama vile Iran, Libya,Somalia,Sudan ,syria na Yemen imeangaziwa katika ujumbe uliotumwa katika balozi zote.

Masharti hayo mapya yalioanza kufanya kazi siku ya Alhamisi yanaelezea mahusiano ya kifamialia kama mzazi, mkeo ama mumeo,mtoto wa kiume ama wa kike.

Masharti hayo yanajiri baada ya mahakama kuu nchini Marekani kuidhinisha kwa muda agizo la rais Trump ambalo lilikosolewa kuwa marufuku kwa Waislamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *