Rais mteule wa Marekani, Donald Trump ameyashambulia mashirikia ya kijasusi nchini humo huku akisema kwamba wangeweza kusababisha uvujaji wa tuhuma kwamba Urusi imekusanya taarifa hatari kumhusu.

Trump ameyasema hayo katika mkutano wake wa kwanza na Waandishi wa habari jijini New York nchini Marekani.

Pia Amevituhumu vile vile vyombo vya habari kwa kutoa taarifa alizoziita kuwa hazina ukweli ambazo amesema zimekusanywa na wagonjwa.

Mashirika hayo ya kijasusi yalimuarifu Trump na rais Obama kuhusu tuhuma hizo wiki iliyopita.

Trump ameendelea kusema kuwa anatarajia kutakuwa na uhusiano mzuri kati yake na Vladimir Putin lakini atahakikisha kwamba Marekani inaheshimika kimataifa kuliko ilivyo sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *