Rais wa Marekani, Donald Trump amewasili nchini Saudi Arabia kwa ziara ya siku mbili ikiwa ni ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu aapishwe kushika wadhifa huo mwanzoni mwa mwaka huu.

Trump anatarajiwa kusaini mikataba minono ya silaha inayokisiwa kufikia Dola za Kimarekani Bilioni 100.

Pia Trump anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa mkutano wa mataifa zaidi ya 50 ya Kiarabu na Kiislamu juu ya mapambano dhidi ya itikadi kali katika Ukanda wa Mashariki ya Kati.

Katika mkutano huo mambo kadhaa yanatarajiwa kuchukua nafasi kubwa kujadiliwa ikiwa ni pamoja na kukua kwa ushawishi wa Iran katika ukanda huo, Vita nchini Syria na Vita dhidi ya kundi la kigaidi la ISIS.

Ziara hiyo itamfikisha Trump nchini Israel ambapo anatarajiwa kujadili mkataba wa nyuklia uliofikiwa mwaka 2015 kati ya mataifa yenye nguvu na Iran, Italy ambapo atakutana na Baba Mtakatifu.

Baada ya hapo anatarajia kuelekea katika mji wa Brussels nchini Ubelgiji atakapohudhuria mkutano wa NATO.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *