Wakili wa rais mteule wa Marekani, Donald Trump ametatua kesi ya mamilioni ya madola iliyokuwa inamkabili mteja wake ili apate nafasi ya kutekeleza majukumu yake mapya na kuangazia changamoto zinazoikabili Marekani.

Trump alikuwa ameshtakiwa na wanafunzi wa zamani kwa ubadhirifu wa pesa katika Chuo Kikuu cha Trump, ambapo wanafunzi walilipa maelfu ya madola kwa masomo baada ya kuwaahidi kwamba watafundishwa siri juu ya uwekezaji.

Rais huyo mteule amekuwa akikanusha madai hayo lakini hatimaye ameamua kulipa dola milioni 25 ili kumaliza kesi hiyo.

Mpango huo hata hivyo haumuhitaji kukiri kwamba alifanya makosa hayo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *