Rais wa Marekani, Donald Trump ameendeleza mgogoro wake na vituo vya runinga nchini humo akisema kuwa vimekuwa na upendeleo na kuonya kwamba atafutilia mbali leseni zao.

Alikasirishwa na ripoti ya ktuo cha habari cha NBC iliodai kwamba kwamba aliwaagiza maafisa wake wa usalama na majenerali kwamba alitaka kuongezwa kwa kiwango kikubwa silaha za kinyuklia nchini humo.

Wiki iliopita NBC iliripoti kwamba waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson alimuita Trump ‘mtu mjinga’ matamshi ambayo Tillerson hajayapinga lakini ambayo rais Trump ameyataja kuwa habari bandia.

Wanahabari wanasema kuwa rais huyo atapata shida kufutilia mbali lesen za vyonbo vya habari.

Lakin baadhi ya makundi ya kupigania haki yanasema kuwa rais Trump anaweka mfano mbaya kwa viongozi wengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *