Rais mteule wa Marekani, Donald Trump ameitaka nchi hiyo kuboresha zaidi uwezo wake wa silaha za nuklia.

Trump amesema kuwa Marekani lazima ichukue hatua kama hizo hadi wakati ulimwengu utatathmini suala la nuklia.

Rais huyo mteule aliyazungumza hayo saa kaadha baada ya rais wa Urusi Vladimir Putin kusema kuwa Urusi inahitaji kuboresha uwezo wake silaha za nyuklia.

Marekania ina silaha 7,100 za nuklia huku Urusi ikiwa inamiliki silaha 7,300 kulingana na shirika la kudhibithi silaha la marekani.

Wakati wa kampeni, Trump amesema kuwa silaha ya nuklia ndilo tatizo kubwa zaidi linaloikumba dunia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *