Rais wa Marekani, Donald Trump amesisitiza kwamba hafanyiwi uchunguzi wowote baada ya kumfuta kazi mkurugenzi wa shirika la ujasusi la FBI.

Trump amesema kwamba ulikuwa uamuzi wake pekee kumsimamisha kazi James Comey.

Comey alikuwa akiongoza uchunguzi kuhusu madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani uliokamilika mbali na uwezekano kwamba kulikuwa na mawasiliano kati ya, maafisa wa Trump na Urusi wakati wa kampeni.

Trump ameutaja uchunguzi huo kuwa unafiki mkubwa madai yaliopingwa na Mrithi wa Comey.

Katika mahojiano yake ya kwanza tangu alipomfuta kazi mkurugenzi huyo , Bwana Trump amesema kuwa kuwa alimuuliza bwana Comey iwapo alikuwa akimchunguza.

Nilimwambia iwapo inawezekana unaweza kuniambia, Je Ninachunguzwa? Aliniambia huchunguzwi.

Rais huyo pia alipinga maelelezo ya ikuu ya Whitehouse kwamba alimfuta bwana Comey baada mapendekezo kutoka maafisa wakuu wa wizara ya haki.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *