Rais wa Marekani, Donald Trump ameomba ufadhili wa ujenzi wa ukuta, kufukuzwa haraka watu kutoka Marekani na kuajiriwa maefu ya maafisa wapya wa uhamiaji.

Mwezi ulioita alifuta mpango wa Obama uliofahamika kama “Dreamer” ambao ulikuwa unawalinda wahamiaji 690,000.

Mwezi uliopita Trump aliliambia bunge la Congress lililo na warepublican wengi kuwa lina miezi sita kukubaliana kuhusu sheria ya kuwasaidia Dreamers.

Hawa ni vijana ambao walipelekwa nchini Marekani kinyume cha sheria kama watoto na hivyo wanakabiliwa na hatua ya kufuzwa kutoka nchini humo.

Chini ya sera za Obama, vijana hao walikuwa na uwezo wa kuomba vibali vya kufanya kazi na kusoma, lakini wakosoaji wanasema kuwa mpango huo ni sawa na kuwapa kinga wahamiaji haramu.

Tangu mpango huo uanze kutekelekwa karibu hali ya wahamiaji 100,000 imebadilika kati ya karibu wahamiaji 690,000.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *