Mkuu wa mikakati wa Rais Donald Trump katika Ikulu ya White House Steve Bannon amefutwa kazi.

Katibu wa mawasiliano na wanahabari katika ikulu hiyo Sarah Huckabee Sanders amethibitisha kwamba Ijumaa ilikuwa siku ya mwisho kwa Bannon kazini.

Kuondoka kwake kumejiri baada ya kutathminiwa kwa wadhifa wake na Mkuu wa Watumishi wa  John Kelly.

Lakini wakosoaji wamemtuhumu Bannon, 63, kwa kuwa na chuki dhidi ya wayahudi na kuwa mtu anayeamini katika ubabe wa wazungu.

Bannon anadaiwa kushindania udhibiti wa ikulu dhidi ya mirengo ya watumishi wenye misimamo ya wastani ikulu, wakiwemo baadhi ya jamaa wa Trump.

Trump alianzisha uvumi kumhusu Bannon alipoulizwa kuhusu mustakabali wake wiki iliyopita lakini akajibu: “Tutasubiri tuone.”

Bannon alinukuliwa akipuuzilia mbali wazo la kutumia jeshi kutatua mzozo kuhusu Korea Kaskazini, jambo lililotazamwa kama kwenda kinyume na msimamo wa Trump.

Bannon amesema kuwa Marekani ilikuwa katika “vita vya kiuchumi na China” na kwamba analenga kuwaondoa watu wenye msimamo wa wastani serikali ya Trump ambao anaamini wana msimamo usio mkali sana dhidi ya China.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *