Rais mteule wa Marekani, Donald Trump amemteua Peter Navarro kuwa kiongozi mkuu wa baraza jipya la kibiashara katika Ikulu ya White House.

Peter Navarro alizindua sera ngumu dhidi ya Beijing na akaandika kitabu kwa jina ‘Death by China: How America Lost its Manufacturing Base”.

Serikali ya mpito ya Doland Trump imemsifu kwa uwezo wake wa kufufua uchumi, mbali na kukabiliana na uhaba wa kazi kwa Wamarekani.

Pia Trump ameteua mwekezaji bilionea na msomi wa uchumi, Carl Icahn kuwa mshauri mkuu wa mageuzi.

Icahn amesema kuwa biashara nchini Marekani, imelemazwa na masharti mengi yasio na maana.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *