Rais mteule wa Marekani, Donald Trump amemteua mume wa mtoto, Jared Kushner kuwa mshauri mwandamizi wa Ikulu ya nchi hiyo.

Kushner mwenye umri wa miaka 35 ambaye amemuoa mtoto mkubwa wa Trump, Ivanka Trump alifanya kazi kubwa wakati wa kampeni za uchaguzi zilizomuwezesha Trump kushinda uchaguzi huo.

Donald Trump: Akiwa na binti yake Ivanka Trum pamoja na mkwe wake Jared Kushner aliyemchagua kuwa mshauri wa Ikulu ya Marekani.
Donald Trump: Akiwa na binti yake Ivanka Trump pamoja na mkwe wake Jared Kushner aliyemchagua kuwa mshauri wa Ikulu ya Marekani.

Majukumu ya kazi yake yanatarajiwa kuhusika na masuala ya sera za nje na ndani ya nchi, ikiwemo masuala ya biashara na Mashariki ya Kati.

Uteuzi huo hauhitaji kuthibitishwa na bunge la seneti la nchi hiyo baada ya kumchagua kushika wadhifa huo.

Lakini hata hivyo baadhi ya wachambuzi wanahoji kama uteuzi huo utakiuka sheria ya kupinga upendeleo wa undugu katika ajira.

Jared Kushner hata chukua mshahara kwa uteuzi huo wa Ikulu ya Marekani na itampa nafasi ya kumfanya kuwa huru na maslahi ya shughuli zake za kibiashara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *