Mgombea wa urais nchini Marekani kupitia chama cha Republican, Donald Trump amemwita mpinzani wake wa chama cha Democratic Hillary Clinton kuwa ni ‘shetani’.

Akizungumza kwenye mkutano huko Pennsylvania bwana Trump alimshambulia Bernie Sanders kwa kumuachia nafasi Bi Clinton kugombea urais kupitia chama cha Democratic.

Mgombea huyo amesema kuwa Sanders alifanya makubaliano na ‘shetani’ kwa kumkubalia agombee urais wa Marekani kupitia chama cha Democratic.

HILLARY

Wanachama wa Democratic na Republican wememkosoa bwana Trump kutokana na matamshi yake kuhusu wazazi wa mwanajeshi M’marekani muislamu aliyeuawa vitani nchini Iraq.

Donald Trump na Hillary Clinton watachuana vikali katika uchaguzi mkuu wa Marekani unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *