Rais wa Marekani, Donald Trump amempigia simu Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na kumpongeza kufuatia ushindi wake kwenye kura ya maoni iliyofanyika Jumapili kwa ajili ya kumuongezea mamlaka.
Rais huyo pia alimpongeza Erdogan kwa kuunga mkono shambulio la Marekani la makombora katika uwanja wa ndege za kivita za Syria mnamo 7 Aprili.
Matokeo yaliyotangazwa baadaye Jumatatu yalionesha asilimia 51.4 ya waliopiga kura waliunga mkono marekebisho ya katiba yaliyokuwa yamependekezwa.
Erdogan alipuuzilia mbali shutuma kutoka kwa waangalizi wa kimataifa kwamba alipendelewa na kampeni ambazo ziliegemea upande mmoja