Rais wa Marekani, Donald Trump amemteua Neil Gorsuch kuwa jaji wa mahakama kuu kwa mwaka mmoja.

Gorsuch mwenye umri wa miaka 49 ni jaji katika mahakama ya rufaa mjini Denver nchini Marekani.

Jaji huyo hatarajiwi kutoa hukumu juu ya utoaji mimba na ndoa za wapenzi wa jinsi moja.

Hata hivyo uteuzi wake unasubiri kuidhinishwa na bunge la Seneti.

Maseneta wa Democratic wametishia kumfungia nje mgombea yeyote atakayeonekana kuwa mhafidhina.

Awali maseneta hao walipinga uteuzi wa watu watatu uliofanywa na rais kuchukua wadhifa wa waziri.

Walisusia vikao vya kuwaidhinisha mawaziri wa fedha na afya waliopendekezwa na kuchelewesha upigaji kura wa kumuidhinisha Jeff Sessions aliyeteuliwa kuwa Mwanasheria mkuu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *