Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa anataka Marekani iimarishe silaha zake za nyuklia.

Trump amesema inaweza kuwa vyema sana iwapo hakungekuwa na taifa lolote lililo na silaha za nyuklia duniani.

Lakini amesema iwapo hilo haliwezekano, basi Marekani itahakikisha kwamba inakuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa silaha za nyuklia.

Ameambia shirika la habari la Reuters kwamba Marekani “imeachwa nyuma sana katika uwezo wake wa silaha za nyuklia”.

Wakosoaji hata hivyo wanasema Marekani na Urusi tayari zina silaha za kutosha za nyuklia kuzuia taifa lolote kushambulia jingine kwa nyuklia.

Marekani ina silaha 6,800 za nyuklia na Urusi 7,000, kwa mujibu wa chama cha udhibiti wa silaha cha Marekani.

Trump amesema kuwa yeye ndiye mtu wa kwanza ambaye angependa kuona kwamba hakuna mtu aliye na silaha za nyuklia, lakini hatutakubali kuachwa nyuma na taifa lolote lile, hata kama ni taifa rafiki, hatutaachwa nyuma katika uwezo wa nyuklia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *