Mgombea urais nchini Marekani kupitia chama cha Republican, Donald Trump amekubali mwaliko wa kumtembelea rais wa Mexico Enrique Pena Nieto leo.

Ofisi ya rais nchini Mexico imesema mipango ya kufanyika kwa mazungumzo ya faragha baina ya wawili hao inakaribia kukamilishwa muda si mrefu.

Mkutano huo utafanyika muda mfupi kabla ya Bw Trump kutoa hotuba kuhusu uhamiaji nchini Marekani.

Enrique Pena Nieto: Rais wa Mexico aliyempa mwaliko mkombea urais wa Marekani kupitia Chama Republican.
Enrique Pena Nieto: Rais wa Mexico aliyempa mwaliko mkombea urais wa Marekani kupitia Chama Republican, Dold Trump.

Bw Trump amewaeleza wahamiaji wa Mexico wanaoingia Marekani kama wahalifu na wabakaji kupitia kampeni zake nchini Marekani.

Trump ameahidi kujenga ukuta kuwazuia wahamiaji kutoka nchini Mexico kuingia nchini Marekani iwapo atachaguliwa kuwa rais kwenye uchaguzi ujao.

Pia rais huyo Pena Nieto ametoa mwaliko kwa mgombea urais wa chama cha Democratic Bi Hillary Clinton.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *