Trump akana wadukuzi wa Urusi waliingilia uchaguzi wa Marekani

0
216

Rais mteule wa Marekani, Donald Trump ametoa shutuma mpya kupinga madai ya ujasusi nchini Marekani kuwa wadukuzi nchini Urusi waliingilia uchaguzi wa Marekani.

Trump aliuliza kuhusu ni kwa nini madai hayo ya udukuzi hayakutolewa kwa umma kabla ya kufanyika kwa uchaguzi.

Kupitia akaunti yake Twitter Trump ameandika “Kabla wadukuzi hawajakamatwa kwenye kitendo, ni vigumu sana kubaini ni nani alikuwa akidukua. Mbona hili halikusemwa kabla ya uchaguzi?”.

Siku ya Ijumaa maafisa wa CIA waliviambia vyombo vya habari nchini Marekani kuwa, wadukuzi wa Urusi walijaribu kuvuruga uchaguzi na kumpendelea Trump.

Trump yuko nyuma ya B Clinton katika wingi wa kura kwa karibu kura milioni 2.8 licha ya yeye kushinda kwa kura nyingi zaidi za wajumbe katika historia ya Marekani.

LEAVE A REPLY