Rais mteule wa Marekani, Donald Trump ametoa ufafanuzi juu ya vipaumbele vyake katika sera zake za kigeni huku akitilia mkazo kwenye biashara na mataifa ya nje.

Trump amesema anataka mipango ya biashara yenye usawa kwa Marekani kutoa mipango yake ya biashara na nchi nyingine duniani hususani China.

Katika uongozi wake anatilia mkazo suala la biashara yenye tija zaidi kuliko biashara huru kama zilizokuwa zinafanyika hapo awali.

Alirudia na kusisitiza kwamba kampuni kubwa za kibiashara nchini Marekani zilizowekeza nje ya Marekani zitakabiliana na ushuru mkubwa wa bidhaa wanazotaka kuuza nchini Marekani.

Trump amesema kwamba angependa Urusi na Marekani wakubaliane kupunguza kwa kiasi kikubwa silaha za kinyuklia kwa kubadilishana na kusitisha vikwazo huko Moscow.

Kwa upande wa Mashariki ya kati amesema mahusiano mazuri yangetakiwa kuundwa nchini Syria na kusimamiwa na washirika wa Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *