Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amesisitiza kwamba hakuna mgawanyiko kwenye kambi yake ya kampeni, licha ya taarifa kudokeza kwamba kuna mzozo mkubwa katika chama hicho.

Akihutubu katika mkutano wa hadhara Florida, Bw Trump amesema kampeni yake inafanya vyema sana.

Vyombo vya habari vya Marekani viliripoti kuwepo kwa mvutano baada ya Trump kurejea matamshi yake ya kushambulia wazazi wa Mwanajeshi aliyeuawa nchini Iraq.

Awali, msaidizi mkuu wake Donald Trump Paul Manaford alikuwa pia amekana taarifa kuwa kuna mgawanyiko mkubwa kwenye kampeni baada ya kile kinachodaiwa mfululizo wa kauli za mgombea huyo wa chama cha Republican, zenye kukwaza.

Baadhi ya Maafisa wa Kampeni za Trump wamesema wanahisi kuwa wanapoteza muda wao.

Hata hivyo, Manafort amemlaumu mpinzani wa Trump wa Chama cha Democratic, Hillary Clinton kwa ripoti hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *