Rais mteule wa Marekani, Donald Trump anatarajia kuanza kutangaza mawaziri watakaofanya kazi katika seikali yake itakayoanza kazi mwezi januari mwakani.

Ripoti zinasema kwamba Trump atamteua mshirika wake wa kibiashara wa zamani Steven Mnuchin kama waziri wa fedha.

Wawili hao walikuwa wanamiliki wa Goldman Sachs, kampuni ambayo Trump aliikashifu wakati wa kampeni zake.

Pia rais huyo mteule ameshiriki mazungumzo na Mitt Romney, ambaye anakisiwa kuwa mwaniaji wa wadhfa wa waziri wa mambo ya kigeni.

Romney aliwania urais kwa tiketi ya chama cha Republican mwaka 2012,kwa wakati mmoja alimwita Trump mtu mdanganyifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *