Wanafunzi watatu wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa kufuatia ajali mbaya ya basi la abiria aina ya Coaster lililobeba wanafunzi na raia kugonga treni katika eneo la TANESCO mkoani Morogoro.

Ajali hiyo imetokea leo alfajiri ambapo Coaster lilikuwa limebeba wanafunzi wengi wa Shule ya Sekondari ya Kayenzi waliokuwa wakienda shuleni pamoja na raia wachache lilipokatiza kwenye njia ya treni na kuligonga.

Imeelezwa pia kuwa treni lililiiburuza Coaster hiyo kwa umbali wa mita 30 kabla ya kusimama hivyo kusababisha vifo hivyo na majeruhi.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Urich Matei, amesema ajali hiyo imetokea leo asubuhi na imehusisha gari aina ya daladala yenye amba za usajili T 438 ADR iliyokuwa inakwenda Mvumi kwenye njia panda inayoingilia treni ndipo ikagonga treni hiyo, na kuburuzwa takribani mita 200.

Kamanda Matei amesema chanzo cha ajali hiyo ni daladala kuingia kwenye njia ya treni bila kusimama ili kuangalia kama kuna treni inakuja, ndipo treni hiyo ikaburuza gari hiyo kwa umbali mrefu na kusababisha maafa hayo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *