Treni ya kifahari ya kitalii ‘Rovols Rail’ kutoka Afrika Kusini leo imewasili nchini Tanzania ikiwa na jumla ya watalii 71.

Treni hiyo ikiwa na watalii hao ilianza safari yake kutoka Afrika Kusini mnamo Machi 1 mwaka huu na kuwasili leo nchini Tanzania.

"ROVOS"/The Pride of Africa "ROVOS"/The Pride of Africa

Wakati wa safari hiyo Treni hiyo imepitia nchi za Botswana, Zimbabwe na Zambia ambapo leo imewasili hapa nchini wakitumia siku 10 kwenye safari hiyo.

Msemaji wa Treni hiyo Querida Vented amesema kuwa wanatarajia kufanya safari hizo  tano mwaka huu huku safari ya Tanzania ikiwa ndiyo safari yao ya kwanza kwa treni hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *