Treni ya abiria iliyokuwa inakwenda mikoa ya Bara imepata ajali usiku wa kumakia leo majira ya katika eneo la Stesheni ya Mazimbu mkoani Morogoro.

Katika hajali hiyo ilihusisha mabehewa saba ambapo manne yakiwa yameegama na matatu yameacha reli.

Abiria mmoja, Ashura Mrisho aliyekuwa anasafiri kwenda Tabora amepata maumivu baada ya kuangukiwa na mizigo ilikuwamo ndani ya behewa moja.

Mabehewa 13 yamerejeshwa Morogoro kuwapangia usafiri mbadala abiria wa treni hiyo ambayo imepata ajali.

Shirika la Reli Tanzania (TRL) linafanya utaratibu wa kuwasafirisha abiria wa bara kwa mabasi hadi Kijiji cha Lukobe Manispaa ya Morogoro ambapo watapanda treni kwenda bara.

Kuhusu wale wa treni ya kuja Dar es Salaam kutoka bara ambayo itasimama Lukobe, watasafirishwa kwa mabasi kurudi Morogoro kuendelea na safari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *