Mkuu wa kampuni ya Uber, Travis Kalanick amejiuzulu katika kundi linalomshauri rais Trump baada ya kukosolewa vibaya na wafanyikazi pamoja na Umma.

Bodi hiyo ambayo pia inamuorodhesha afisa mkuu wa kampuni ya Tesla Elon Musk inatarajiwa kukutana na rais leo.

Uber ni miongoni mwa kampuni za teknolojia zilizo na wasiwasi kuhusu athari za marufuku ya uhamiaji kwa nguvu kazi yake.

Kampuni hiyo imesema kuwa imeanzisha hazina ya dola milioni 3 kuwasaidia wale ambao wameathiriwa.

Hata hivyo Elon ametuma ujumbe katika mtandao wake wa Twitter akisema atahudhuria mkutano wa leo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *