Mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz jana ameitwa kwenye ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuelezea chanzo cha mapato yake na ulipaji wa kodi.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Diamond Platnumz ameandika kuwa aliitwa na maafisa wa kodi kuelezea vyanzo vyake vya mapato namna gani analipa kodi kutokana na mapato hayo anayoingiza kwenye kazi yake ya muziki.

Mamlaka hiyo iliamua kumuita Mwanamuziki huyo ili kujua analipaje kodi kutokana na mapato yake anayoingiza kutokana na muziki wake ambapo ndiyo chanzo cha mafanikio yake kwasasa.

Lakini Diamond ajaeleza jinsi ulipaji kodi wake unavyokuwa licha kuweka picha hiyo huku akieleza kama aliitwa na Mamlaka hiyo inayohisika na mapato nchini.

Hii na mara ya pili kwa  Diamond kuitwa ofisi za Serikali baada ya wiki iliyopita aliitwa na kamanda wa Polisi kikosi cha Usalama barabarani, Mohamed Mpinga alipotakiwa kuripoti baada ya kutupia video iliyomuonyesha akiendesha gari huku akiwa hajafunga mkanda.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *