Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imetenga eneo la biashara la Kariakoo Jijini Dar es salaam kuwa Mkoa Maalum wa Kodi kutokana na kuwa kitovu cha biashara hapa nchini.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi kutoka TRA, Bwana Richard Kayombo amesema uamuzi huo umefikiwa kutokana na eneo hilo kuwa na wafanyabiashara wengi watanzania na wengi wa nje kufuata mizigo na kufanya biashara katika eneo hilo.

Pia Kayombo ameongeza kuwa kuna tabia ya baadhi ya wafanyabiashara ambao wamekuwa wakiuza mizigo na kutoa risiti bandia kwa wateja kwa kukubaliana lengo likiwa ni kuinyima serikali mapato hivyo jambo hilo litashughulikiwa kwa urahisi zaidi kuliko hivi sasa.

Pamoja na hayo Kayombo amewataka wananchi kujitokeza katika vituo vya TRA vilivyopo maeneo mbalimbali nchini kuhakiki TIN zao za biashara kabla ya tarehe 15 Oktoba na muda huo ukipita hautaongezwa kwa ajili ya kazi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *