Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Kwa kushirikiana na Ubalozi wa China hapa nchini imeandaa semina Kwa ajili ya Jumuiya ya Wafanyabiashara wa China kuhusu utoaji elimu juu ya kutambua mambo ya kodi na uwekezaji.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu Kwa mlipa kodi, Richard Kayombo amesema kuwa elimu hiyo itakayotolewa ya mlipa kodi itahusisha namna ya kuzingatia na kuzitumia sheria za kutoza kodi sahihi na kukokotoa kodi ya zuio katika bidhaa na huduma na hivyo kuongeza ulipaji wa kodi Kwa hiari miongoni mwao.

Amefafanua kuwa katika semina hiyo kutakuwa na mada mbalimbali ikiwemo kutambua mabadiliko ya Bajeti 2016/17, masuala ya forodha,na uondoshaji wa bidhaa, kodi ya zuio hususani katika sekta ya ujenzi na kodi ya ajira ambapo wafanyabiashara hao watapata fursa ya kuuliza maswali na kupatiwa ufafanuzi ili kuwawezesha kufanya shughuli zao Kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

Aidha katika semina hiyo waziri wa viwanda na biashara anatarajiwa kufungua semina hiyo ambayo pia itahudhiriwa na Balozi wa China hapa nchini na zaidi ya wafanyabiashara 200 wa China wanatarajiwa kuhudhuria.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *