Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanzisha utaratibu wa kufungua klabu za wanafunzi wa kodi vyuoni ili kurahisisha utoaji na upatikanaji wa elimu kwa mlipa kodi katika jamii.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi kutoka TRA, Richard Kayombo wakati akizungumza na wanafunzi wa Chuo kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro.

Kayombo amesema kwamba lengo la kuanzisha Klabu hizo ni kutaka kuwajenga wanafunzi kuwa na misingi ya ulipaji kodi.

Pia mkurugenzi huyo amewaambia wanafunzi hao kwamba wanavyonunua bidhaa wanakuwa wanachangia kodi, kama wanafunzi wote vyuo vyote nchini siku moja wakasema katika manunuzi yenu kila mtu anayenunua adai risiti au wakasema usipo toa risiti tunasusa hatununui kwako wote ana hakika watatoa risiti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *