Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imezifungia ofisi za Shirikisho la Soka nchini TFF kutokana na deni la kodi wanaodaiwa shirikisho hilo.

Kampuni ya Udalali na Minada ya Yono, ndiyo imezifunga ofisi hizo na kwa sasa ndiyo inazishikilia ofisi hizo baada ya kuwatoa nje wafanyakazi wote wa TFF na kuwataka waache kila kitu ndani.

Madeni wanaodaiwa ni ya tangu uongozi uliopita, chini ya rais, Leodegar Tenga kabla ya uongozi wa sasa, chini ya Rais Jamal Malinzi kuingia madarakani.

Deni wanalodaiwa na TFF na TRA linatokana na kodi za mishahara ya aliyekuwa kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Marcio Maximo kwa miaka minne tangu 2006 hadi 2010.

Huku deni lingine linalosababisha ofisi za TFF kufungwa ni la kodi ya Ongezeko la Thamani (VaT) la ziara ya timu ya taifa ya Brazil nchini mwaka 2010 ilipokuwa njiani kwenye Afrika Kusini kwenye fainali za Kombe la Dunia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *