Kiungo wa Ujerumani, Toni Kroos amesaini mkataba mpya na klabu yake ya Real Madrid utakao muweka bernabeu mpaka msimu wa mwaka 2022.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 alijiunga na Real Madrid msimu wa mwaka 2014 akitokea katika klabu ya Bayern Munich kwa ada ya uhamisho iliyogharimu kitita cha paundi milioni 24.

Kroos toka ajiunge na Real Madrid amefunga goli nne baada ya kucheza michezo 108 katika mashindano tofauti inayoshiriki klabu hiyo yenye maskani yake Bernabeu.

Kutokana na mkataba huyo aliosaini kiungo huyo atakuwa analipwa Euro 346,000 kwa wiki kutokana na mkataba huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *