Tommy Flavour ajipu tuhuma za Alikiba kuiba wimbo

0
76

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Tommy Flavour amekanusha taarifa za kuiba wimbo wa sitaki tena inayopatikana kwenye Album ‘Only One King’ ya Alikiba kwa kusema haijawahi kutokea kumdhulumu mtu wimbo wake.

Tommy Flavour amesema hayo baada ya kusambaa taarifa kuwa Alikiba alitumia wimbo wa mtu kwenye albam yake mpya iliyotoka juzi.

Msanii wa Mesen Selekta Liah alidai haki zake za kukopiwa verse na melody zinazopatikana kwenye wimbo wake wa doa aliyoitoa miaka miwili iliyopita kutumiwa na Alikiba ambapo muandishi wa hiyo ngoma ni Tommy Flavour.

Alikiba mwenyewe bado ajajitokeza hadharani kujibu tuhuma hizo zinamuandama za kuiba wimbo wa msanii mdogo na kuuweka kwenye albam yake mpya.

LEAVE A REPLY