Bendi mpya ya Taarab nchini, TMK Modern Taarab inatarajia kufanya uzinduzi rasmi wa bendi hiyo katika ukumbi wa Dar Live ifikapo Desemba 17 mwaka huu.

Bendi hiyo inamilikiwa na Said Fella wa Mkubwa na Wanawe ambaye ni mdau mkubwa wa muziki wa Bongo fleva ambaye sasa ameamua kugeukia muziki wa Taarab baada ya muziki huo kuonekana kushuka kwasasa.

Kundi hilo limekusanya wasanii mbali mbali kutoka bendi tofauti za taarab nchini ikiwemo bendi ya Taarab ya Jahazi Modern Taarab.

TMK Modern Taarab hadi sasa ina jumla ya nyimbo mbili ambazo zipo tayari ambazo ni Bi. Sina Pupa iliyoimbwa na Mwanahawa Ally pamoja na Kibaya kinamwenyewe iliyoimbwa na Aisha Vuvuzera.

Wasanii wengine waliomo kwenye bendi hiyo ni Mohamed Mauji na Chidy Boy waliokuwa Jahazi Modern Taarab, Babu Ali, Fatma Mcharuko na Maua Tego.

Uzinduzi wa bendi hiyo utafanyika katika ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam ifikapo Desemba 17 mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *