Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) imetahadharisha kuchelewa kwa mvua za vuli na kusema hata zitakazonyesha, zitakuwa ni za wastani au chini ya wastani katika maeneo mengi ya nchi katika kipindi kinachoanzia Oktoba hadi Desemba mwaka huu.

 Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi amesema mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli nchini zitachelewa kwa kipindi cha Oktoba hadi Desemba mwaka huu

Dk Kijazi amesema kuanza kwa vuli kunatarajiwa kuwa na vipindi vikavu katika maeneo mengi hususan katika miezi ya Oktoba na Novemba. Imesema kutokana na hali hiyo, hali ya unyevunyevu katika udongo inatarajia kuwa si ya kuridhisha kwa ustawishaji wa mazao ya kilimo na malisho kwa mifugo.

Mamlaka hiyo imewashauri wakulima kuandaa mashamba na pembejeo mapema pamoja na kuzingatia ushauri wa maofisa ugani wa kilimo kwa matumizi sahihi ya ardhi na mbegu, pia kutumia kwa uangalifu na kuhifadhi akiba ya chakula walichonacho.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *