Mwanamuziki nyota wa Nigeria, Tiwa Savage anatarajia kutumbuiza kwenye wiki ya kuelekea utoaji wa tuzo za Grammy jijini Los Angeles Februari 9 mwaka huu.

Kupitia akaunti yake ya Instagram mkali huyo ameweka picha ikionesha tangazo la yeye kufanya show kwenye tuzo hizo kwenye kipengele kijulikanacho kama ‘Black Women in Music’.

grammy

Tiwa Savage anakuwa mwanamuziki wa pili kutoka Nigeria kupata nafasi ya kutumbuiza kwenye sherehe hizo kubwa za utoaji tuzo za muziki nchini Marekani baada ya mwanamuziki mwenzake Yemi Alade kupata mwaliko wa kuhudhuria tuzo hizo.

Tuzo za Grammy ni tuzo kubwa za muziki nchini Marekani ambapo kila mwanamuziki ana hamu ya kushiriki tuzo hizo hata kama hatoshinda lakini kushiriki ni heshima pia na zinatarajiwa kufanyika Februari 12 mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *