Nyota wa muziki kutoka Nigeria, Tiwa Savage amerudiana na mumewe Teebillz baada ya kuachana naye kwa kile kilichodaiwa kuwa mwanamme huyo anatumia madawa ya kulevya.

Teebillz  amefanikiwa kutibiwa kisiri katika kliniki ya tiba ya madhara yatokanayo na matumizi ya madawa ya kulevya pamoja na kufanyiwa ushauri wa masuala ya ndoa (Drug Addiction Rehabilitation & Series Of Marriage Counselling).

Tiwa amerudiana na mumewe huyo kimya kimya bila watu kujua kwa kile alichokieleza kuwa afya ya mumewe huyo inaendelea kuimarika baada ya kutibiwa utumiaji wa madawa ya kulevya uliokuwa umemuathiri kwa kiwango kikubwa.

Sababu nyingine ni kwamba wanataka wamlee kwa pamoja mtoto wao wa kiume aitwae Ajmil.

Wawili hao wamekuwa wakionekana kwa pamoja wakienda kwenye kituo kimoja cha ushauri wa masuala ya kisaikolojia na mambo ya ndoa jijini Lagos kwa ajili ya kupata ushauri nasaha kuhusu ndoa yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *