Baada ya kimya kirefu wachekeshaji maarufu nchini, Tin White na Ringo wameachia filamu yao mpya inayoitwa ‘Kombando Kipensi’.

Wachekeshaji hao mara nyingi wamekuwa wakiigiza pamoja wamesema filamu hiyo itakuwa ina mapigano ndani yake.

Pia wachekeshaji hao wamewataka mashabiki wao kuinunua filamu hiyo kutokana na kuigiza tofauti na filamu zao nyingine za hapo awali.

Tin White amesema kwamba filamu hiyo ni ya kuchekesha lakini ndani yake kuna ngumi na mapanga huku akisisitiza kuwa ni filamu kali sana na leo imeingia sokoni kwa hiyo kila mmoja akanunue nakala yake.

Wachekeshaji hao kwasasa wana show yao inayooneshwa na kituo cha Azam TV inayoitwa ‘Mahoka’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *