Timu zinazoshiriki ligi kuu Tanzania Bara zinatarajia kukabidhiwa vifaa mbalimbali kwa ajili ya msimu mpya wa ligi hiyo siku ya Alhamisi katika hafla fupi itakaofanyika LAPF tower Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Meneja uhusiano wa Vodacoma, Matina Nkurlu amesema zoezi la kukabidhi vifaa  vya michezo kwa msimu ujao utakaoanza kutimua vumbi mwezi huu tarehe 20 lipo tayari kabisa na litafanyika tarehe 4 siku ya alhamisi.

Matina Nkurlu amevitaja vifaa vitakavyokabidhiwa kuwa ni jezi, viatu vya mazoezi na mechi, mipira, soksi, vilinda ugoko, nguo za mazoezi, nguo za kawaida, gloves na vifaa vingine vinavyohitajika,vyote kwa pamoja kwa mujibu wa mkataba.

Meneja huyo amesema kwamba vifaa vyote kwa ajili ya ligi ya msimu ujao vipo tayari kilichobakia ni kuvikabidhi siku ya alhamis ili timu ziweze kuendelea na maandalizi mengine kabla ya ligi kuanza mwishoni mwa mwezi August.

Pia amesema hafla hiyo ya kukabidhi vifaa inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa Shirikisho la Soka,Viongozi wa klabu mbalimbali vinavyoshiriki katika ligi,wachezaji kutoka timu mbalimbali bila kusahau wadau wengine wa soka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *