Timu ya Tenisi ya Walemavu ya Tanzania imefanikiwa kufuzu kushiriki michuano ya Dunia BNP Paribas baada ya kuifunga Kenya kwa Seti 2-0 katika mchezo wa Fainali wa mashindano ya kufuzu ya Afrika yaliyofanyika nchini Kenya.

Kocha Mkuu wa Timu hiyo Riziki Salum amesema, wamefurahi kuibuka na ushindi na kufanikiwa kuiwakilisha Afrika kwa upande wa wanaume katika michuano ya Dunia.

 Salum amesema, kwa upande wa timu ya wanawake imefanikiwa kuibuka na ushindi wa pili baada ya kufungwa na Kenya.

Kocha huyo aliwataja wachezaji walioshiriki mashindano hayo kuwa ni Novatus Temba, Juma Hamis, Jumanne Nassor huku kwa upande wa wanawake wakiwa ni Rehema Seleman na Lucy Julius.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *