Wachezaji wa timu ya taifa ya riadha ya Tanzania watakaokwenda kushirikia michuano ya olimpic wamendelea na maandalizi ya mwisho katika kambi yao iliyopo mkoani Kilimanjaro kabla ya kuelekea nchini Brazil kushiriki michuano hiyo.

Tanzania itawakilishwa na wanariadha wanne katika michuano hiyo, ambao ni Alponce Felix, Fabiani Joseph, Saidi Juma pamoja na Sara Ramadhani.

Kocha wa kikosi hicho Francis John amesema kwamba wamekaa miezi saba kambini wakijiandaa na michezo hiyo mikubwa hivyo wanamatumaini makubwa watafanya vizuri na kurudi na medali.

Michezo ya olimpic itaanza kutimu vumbi kuanzia tarehe 5 Agosti na kufikia tamati Agosti 21 katika mji wa Rio de Janeiro nchini Brazil, jumla ya mataifa 207 yatashirishiki katika matukio 306 ya michezo 28 tofauti.

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *