Wachezaji wa klabu ya Ruvu Shooting wamepata ajali mkoani Singida wakiwa safarini kurejea Dar es Salaam baada kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Stand United.

Aajli hiyo imetokea baada ya gari likiwa katika mwendo wa kasi kiasi ndipo tairi likapasuka na kusababisha gari kuhama njia na kuparamia miti iliyokuwa jirani mwa eneo hilo.

Katika ajali hiyo hakuna mtu yeyote aliyepata majeraha makubwa katika tukio hilo, isipokuwa mchezaji mmoja ambaye amepata majeraha ya kawaida.

Ruvu Shooting ilikuwa mkoani Shinyanga ilipocheza mechi ya mwisho ya Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/17 dhidi ya Stand United na kupoteza kwa mabao 2-1.

Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo maeneo ya Manyoni mkoani Singida.

Gari hiyo iliacha njia kama mita 400 kutoka barabarani iliyosababishwa na taili ya mbele kupasuka.

Wachezaji walioumia ni Yussuf Nguya, Abdul Mpambika na Saidi Dilunga ambao wamepata majeraha ya kawaida.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *