Mechi za mwisho za kufuzu kombe la Mataifa ya Afrika zimehitimishwa jana ambapo timu 16 zimekata tiketi ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika itakayofanyika Gabo mwakani.

Timu 16 ambazo zitashiriki michuano hiyo mwakani ni Gabon ambaye ni mwenyeji

nyingine ni Algeria, Burkina Faso, Cameroon, Ivory Coast, DRC, Misri, Ghana, Guinea Bissau, Mali, Morocco, Senegal, Togo, Tunisia, Uganda na Zimbabwe.

Uganda iliyomaliza nafasi ya pili Kundi D kwa pointi zake 13, na Togo, ya pili Kundi A kwa pointi zake 11 wamefuzu kama washindi wa pili bora.

Guinea-Bissau itakuwa nchi pekee inayoshiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza kabisa wakati Senegal imekuwa timu pekee iliyoshinda mechi zote sita za kundi lake.

Mashindano hayo hufanyika kila baada ya miaka miwili ambapo mwakani yatafanyika nchini Gabon huku Ivory Coast akiwa bingwa mtetezi.

 

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *