Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Timbulo amesema kuwa label ya QS Mhonda haijui jambo lolote kuhusu muziki na kushauri kuwa ni bora waelekeze nguvu zao katika masuala ya ujenzi kwani huko ndiko wanaweza kufanya vizuri.

Hayo yameibuka hivi karibuni baada ya wimbo alioshirikiana na Patoranking kutoka nchini Nigeria uliopewa jina la ‘Koku’ kuvuja na kwamba vionjo vile vinavyopatikana kutoka kwa wasanii ambao wanasimamiwa na uongozi huo wa QS.

Kolabo ilifanikishwa na QS Mhonda, jambo lililozua hisia kuwa huenda QS akawa amehusika au amemjumuisha Timbulo katika label yake.

Aidha msanii huyo amesema hawezi kuingia QS kwa kuwa hawezi kukuza kipaji alichonacho maana ameona mifano hai kutoka kwa wasanii wake aliyokuwa nao kushindwa kufikia malengo yao na hatimaye kumkimbia sasa.

Kwa upande mwingine Mhonda amekanusha taarifa za kupata barua ya shukrani kutoka kwa aliyekuwa msanii wake Q-Chief.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *