Kampuni ya Tigo inatakiwa kuwalipa wanamuziki wa Bongo Fleva, Mwana FA na AY kiasi za bilioni mbili baada ya wasanii hao kushinda kesi dhidi ya kampuni hiyo ya simu nchini.

Hukumu hiyo imetolewa na mahakama Kuu ya Tanzania baada ya kutupilia mbali rufaa iliyofunguliwa na kampuni hiyo kupinga kuwalipa wasanii hao baada ya kutumia nyimbo zao bila kuwalipa.

Akizungumza baada ya hukumu hiyo Wakili wa wasanii hao, Albert Msando amesema huu ni ushindi muhimu kwa sanaa ya Tanzania kwani ni haki yao kulipwa kwa sababu ni kazi zao ambazo zinalindwa kisheria.

Mnamo mwaka jana Mahakama Wilaya ya Ilala, iliamuru kampuni ya MIC Tanzania (Tigo) kuwalipa wasanii hao kiasi hicho cha fedha kutumia nyimbo zao bila idhini.

Kampuni hiyo ilibainika kutumia nyimbo za wasanii hao kwa kipindi tofauti kama miito ya wateja wao na kufanya biashara bila idhini ya wasanii husika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *