Mkali wa Bongo Fleva, TID amesema kuwa atawachukulia hatua watu wanaosambaza taarifa kuwa amepewa pesa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makondaili ataje majina ya wanaohusika na dawa za kulevya.

 

TID amefunguka na kusema kuwa yeye alikuwa ni muathirika wa dawa za kulevya na serikali ilimkamata kwa kosa la kutumia lakini ikaamua kumsaidia kwa kumfanya aachane na dawa hizo pamoja na kumpa nafasi ya kuelimisha vijana wenzake ambao bado wapo katika janga hilo.

 

TID ameonesha kushangazwa na kuumizwa na taarifa zinazoenea kuwa amepewa pesa ili ataje watu au ajitangaze, jambo ambalo amesema ni wivu wa baadhi ya watu wasiomtakia mema, na wanaotaka kumuona akiendela kutaabika kwenye matumizi ya dawa hizo.

 

Msanii anayedaiwa kutoa kauli hiyo ya TID kupewa pesa ni Steve Nyerere, kupitia sauti za simu zilizosambazwa tangu juzi, zikionesha mtu anayedhaniwa kuwa ni Steve Nyerere akiongea na mtu anayedhaniwa kuwa ni Mama wa Msanii Wema Sepetu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *