Mwanamuziki wa Bongo Fleva, TID a.k.a Mnyama amesema kuwa kukaa mahabusu kwa  wiki nzima kitu kilichomuathiri zaidi.

TID amesema kuwa mahabusu kuna watu mbalimbali wakiwamo wahalifu wa aina tofauti ambao walimbugudhi kwa vile yeye ni maarufu na kwamba kimsingi jambo hilo lilimkwaza sana.

Hata hivyo, alimshukuru Makonda kwa kampeni yake ya kupambana na dawa za kulevya kwamba imefungua ukurasa mpya kwake.

 TID amefafanua kuwa mara nyingi alikuwa akikana kutumia dawa za kulevya lakini baada ya kukiri na kusaidiwa wiki tatu zilizopita anaona mafanikio makubwa mbele yake.

Amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwa sababu sasa ameamua kufuatilia kazi zake alizokwisha kuziandaa lakini alishindwa kwa sababu ya matumizi ya dawa kulevya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *