Mshambuliaji wa Taifa Stars, Thomas Ulimwengu anatarajia kwenda nchini Uholanzi kufanya mazungumzo na klabu ya huko baada ya kuletwa ofa inayomuhitaji mchezaji huyo wa zamani wa TP Mazembe.
Hayo yamesemwa na wakala wake, Jamal Kisongo ila amesema kwa sasa asingeweza kuitaja timu hiyo, hadi siku ya Jumatano, pamoja na ofa nyingine zilizopo mezani hadi sasa.
Meneja huyo amesema kuna matarajio ya Ulimwengu kupata timu Ulaya na amewataka Watanzania wawe wavumilivu na kumuombea kijana huyo ili afanikiwe kucheza Ulaya.
Thomas Ulimwengu aliachana na klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kumaliza mikataba yao mwaka uliopita.