Mchezaji wa Taifa Stars, Thomas Ulimwengu ameondoka katika klabu yake ya TP Mazembe baada ya kudumu kwenye klabu hiyo kwa miaka mitano.

Mchezaji huyo alichukuliwa na klabu hiyo akiwa na umri 18 kutoka AFC Academy ya Stockholm, Sweden.

Akiwa na TP Mazembe, Ulimwengu amecheza mechi 130 na kufunga mabao 35 toka ajiunge nayo.

Ameamua kutoongeza tena mkataba na TPM. Na sasa Ulimwengu anataka kufuata nyayo za Mtanzania mwenzake Mbwana Samatta wa Genk ya Ubelgiji.

Kabla ya kuondoka Lubumbashi, Ulimwengu amesema miaka mitano Mazembe imemruhusu kuendelea kukua kisoka na anataka kuwashukuru wote waliomuunga mkono na kusaidia kushinda vikombe wakiongozwa na Rais Katumbi na Mrs Carine, viongozi na makocha.

Ulimwengu anafuata nyayo za mchezaji mwenzake wa Taifa Stars Mbwana Samatta ambaye walikwa wakicheza timu hiyo ya TP Mazembe ambaye kwasasa anachezea klabu ya Genk nchini Ubelgiji.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *